Wednesday, 28 December 2016

UMARIDADI WA KUPAKA KUCHA RANGI.


Ili uwe na kucha maridadi masuala ya kuzisafi na kuziweka rangi ni muhimu ama sivyo? na kwa kawaida kucha zilizo safi ndizo hasa zinazokubali polishi yaani rangi au sivyo?
Na ama hakika kucha zilizo safi ndizo hasa zinazotengenezwa na kuwekwa sopusopu.
Ni vyema kutambua kwamba wakati wa kupaka rangi tumia mipako michache kwa kila mpako na kila mpako uachie ukauke kabla ya kuanza mpako mwingine.
Na ile ya mwisho inatakiwa kuwa bomba zaidi kwa kuwa ndio hasa itakayokuwa inatunza matabaka mengine yote.
Utengenezaji mzuri wa kucha si lazima uwe wa kwenda katika mapumziko au kuonyesha mtu ni kitu ambacho kinafaa kufanywa ili uwe mrembo kila mahali.
Kuna raha ya kujisikia katika rangi mpya katika mwaka mzima na hasa kama uchaguzi wako wa rangi za kupaka ni bomba.
Moja rangi ya pinki ama nyekundu inakupa nafasi ya kuwa funny . Unaweza kujipaka rangi mwenyewe au kuwambia mtu akupake rangi.Kuna hatua kadhaa ambazo unatakiwa kuzifanya kabla ya kupaka rangi kucha zako.
Hatua ya kwanza ni kuondoa rangi zote za awali.kwa kufanya hivyo rangi mpya itakuwa ina uwezo wa kushika katika kucha.
Pia kunasaidia rangi yako mpya isitibuliwe na rangi ya zamani kwa namna yoyote ile.
Unaweza kuondoa rangi ya zamani kwa kutumia dawa inayopatikana katika maduka ya dawa na hata yale ya vipodozi na pamba hufanya vyema kartika kuondoa rangi za kucha kwa kutumia Nail polish remover.
kazi ya pili ni kutafuta rangi inayokupendeza. unaweza kutumia rangi yoyote kwa sababu mara nyingi viatu vinazuia kuonekana kwa kucha zako la kama unahitaji rangi fulani kwa sababu miguu yako i wazi ni vyema sana.
Tazama kwamba vipaka rangi vyenyewe ni vipya kwani vilivyozeeka huleta tatizo kidogo.mara nyingi vipaka rangi vilivyokaa miaka miwili havifai tena kutumika.
Anza kupaka baada ya kubainisha kwamba unaweza kutenganisha kidole kwa kidole ili usipake kila mahali hasa kama brashi husika ni pana kidogo.
Anza katikati kwa kuanzia nyuma kupeleka mbele kisha nenda pembeni na pembeni.Na baada ya kukauka unaweza kuongeza tabaka jingine tena na tena.
Kisha paka ile ya mwisho ambayo ndiyo italinda rangi yenyewe yaani top coat . top coat husaidia sana kuweka rangi kwa muda mrefu. Top coat ni polishi isiyokuwa na rangi na kama unataka kuweka stika iweke mapema kabla ya kuweka top coat.
rangi nzuri na zilizotulia zinakufanya uwe na sababu ya kujivalia sandals zako nzuri au viatu vya wazi

No comments:

Post a Comment