Ukiwa mwanaume au mwanamke upigaji sopusopu ni jambo la busara sana ili
kukuweka mtanashati na mwenyekuvutia muda wote kwa kuondoa uchafu na pia
kuondoa mafuta ambayo yana kawaida ya kutanda katika sura.
Kitendo hicho huitwa scrub.Husaidia kuondoa chunusi,vipele na makovu na pia inapunguza mafuta usoni.
Uso
unapokuwa na mafuta sana na kuyaondoa kunasaidia kupunguza vitu vingi
pamoja na vipele na hata mabaka yaliyosababishwa na vipele au chunusi.
Unaweza kutumia scrub ya kwa njia ya mikono kwa kila baada ya siku tatu, na scrub ya mashine baada ya mwezi mmoja.
Scrub
ya mkono.Tafuta aina ya scrub inayokufaa kulingana na ngozi
yako.safisha uso wako mpaka uhakikishe kuwa umetakata kisha chukua scrub
na kuanza kusugua usoni taratibu kwa muda wa dakika tano kisha nawa uso
na unaweza kupakalosheni au poda baada ya kunawa.
Scrub ya mvuke.Chesha maji Nawa uso kwa kutumia maji safi na uhakikishe kuwaumetakata.
Futa uso kwa kutumia taulo safi.
Paka
scrub usoni na pia shingoni kama utapenda. Sugua uso kwa kutoa
taka.Chukua taulo jifunike na kisha inamia beseni lenye maji ya
moto.Baada ya dakika tano toka na subiri kwa muda wa dakika tano
nyingine kisha nawa. Paka poda au losheni.
Pia unaweza kutembelea
saluni za kisasa kwa ajili ya kuufanyia facial uso wako Pia unaweza
kutafuta sabuni ya ukwaju na ukawa unanawa uso asubuhi na jioni hii
huondoa upele, chunusi na mabaka usoni
No comments:
Post a Comment