Leo katika somo letu la urembo ningependa kuangalia katika utunzaji wa
nywele bila ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya kemikali ambayo
yamesababisha kwa kiwango kikubwa matatizo katika ukuaji wa nywele kama
nywele kukatika,kunyonyoka,kupooza katika ukuaji n.k
Hebu tuanze maandalizi ya Hina.
MAHITAJI:-
- Hina vijiko vitatu vya chakula.
- Kipande cha ndimu au limao.
- Maji ya chai kiasi kidogo.
- Glavu mbili mpya.
NAMNA YA KUFANYA:-
- Vaa glavu ili mikono yako isiharibiwe na hina.
- Changanya hina na viungo vyake hakikisha haiwi nyepesi sana wala nzito sana.
- Gawa nywele zako katika mafungu manne,kisha paka hina yako kwa uangalifu ili isichafue uso wako.
- Hakikisha unakaa nayo kwa muda usiopungua lisaa limoja.
- Zikiwa tayari,hakikisha unaosha vizuri na kukausha nywele zako kwa taulo lililo safi.
Ningependa kukushauri kutumia mafuta yasiyo na kemikali yatokanayo na vitu asili kama mimea, matunda nk.
No comments:
Post a Comment