Sasa leo nimekuja na TIPS chanche za kukufanya wewe uonekane mrembo zaidi kila wakati .
1. USO -
osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu na sabuni. kausha vzuri na kitaulo laini.
kama unatumia cleanser yoyote ni vizuri zaidi kuondoa uchafu kwenye uso
wako kwa kutumia pamba na baada ya hapo osha tena uso wako kwa maji tuu
ya uvuguvugu na ujikaushe.
2. FOUNDATION
Chagua faoundation inayoendana na rangi ya ngozi yako,
foundation ndo ya kwanza
kupaka usoni kwako ili kuziba vidoa doa vilivyo kwenye ngozi ya uso wako
,paka kwa kutumia brush maalum ukianzia katikati kwenda chini na
juu.epuka kuanzia kwenye pji la uso yani nywele zinapoanzia kwani
itasbabisha mlundikano.
3. POWDER
Paka powder inayoendana
na ngozi yako juu ya foundation,hakikisha unasambaza uso wako wote
pamoja na sehemu za shingo ili rangi iwe sawa na uso. kwa kutumia
spounge au brush inayohusika.
NB: ZINGATIA SANA RANGI YA PODA PAMOJA NA RANGI YA NGOZI YAKO ,KWANI UNAWEZA UKAWA MNG'AVU THEN UKAPAKA PODA AMBAYO ITAKUFIFIZA
No comments:
Post a Comment