Wanawake wengi kwa
sasa wanakwenda kuboresha makalio yao ili kuyapatia ukubwa unaostahili kwa
jinsi wao wanavyopenda.
Tatizo hili halipo
hapa nchini lakini wapo walionituipia swali sasa inabidi nikiri kuwa lipo sana
marekani na mpasuaji wa masuala ya urembo wa Miani Dk Costantino Mendieta
amethibitisha.
Katika fasihi yake
mtaalam huyo amezungumzia sana utunzaji wa makalio kwa kuyagawa katika madaraja
manne.
Anasema makalio
daraja la kwanza ndiyo yanayotakiwa sana > Ni kama vile umechukua moyo
halafu ukaugeuza chini juu haya ndiyo dizaini ambayo Marekani wanalilia sana.
Watu wa huko wanajimwaga katika majumba ya upasuaji kupata shepu hiyo adimu.
Hatua hizo ni kama ifuatavyo.
1.fanya masaji na
losheni zinazoimarisha na kutengeneza ngozi mwororo katika mapaja yako ukianzia
chini ya makalio mara mbili kwa siku.
2.Ondoa miinuko
midogo midogo isiyotakiwa ni yako kwa kuskrabu mara mbili au tatu kwa wiki
ukitumia salt scrub.
3.Pamoja na
matatizo ya michuchumio, ivae ili kukupa nafasi ya kutembea kwa miondoko ya
twiga inayotoa nafasi nzuri kwa makalio kuwa na mvuto.
4.tafuta namna
nzuri ya kuficha michirizi ya kunyooka kwa misuli ya mwili.
5.Mazoezi
yatakufanya uwe mtu tofauti zaidi pandisha ngazi kwa dakika kumi au zaidi na
chukua mazoezi ya kubana makalio yako na sehemu za kiuno kwa kusukuma kwa ndani
na kutulia hivyo kwa sekunde tano na kujiachia na unaweza kufanya hivyo
unavyotaka.
Pia unaweza
kuongeza uzuri wa makalio yako kwa kuhakikisha unakula vyema na unakula
inavyostahili.
No comments:
Post a Comment