HAIJALISHI unafanya kazi kwenye mazingira gani lakini cha muhimu ni
kuzingatia unatunza vizuri ngozi yako ya uso ili kuboresha muonekano
wake.
Mwanaume kuwa na ngozi nzuri huleta, furaha na kujiamini pia .
Muonekano mzuri usoni ni miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanatakiwa
kuyazingatia na hili linawezekana kama utaijali ngozi yako na utanashati
kwa jumla.
Kuna wanaume ambao hawana hata muda wa kujiangalia kwenye kioo labda kwa
kudhani kuwa mambo hayo yanatakiwa kufanywa na wanawake jambo ambalo si
sawa sawa.
Kuna mambo mengi ambayo mwanaume anatakiwa kufanya ili aweze kuonekana
na muonekano mzuri.
Miongoni mwa mambo hayo ni kuhakikisha unasafisha uso na kutakata, hapa
unaweza kutumia taulo laini kwa kupaka kidogo sabuni na kisha safisha
uso taratibu na baadaye unasuuza uso na kuufuta.
Pia unaweza kutumia cleanser ambayo ni maaluma kwa ajili ya kusafisha
uso.
Si jambo la ajabu unapopita kwenye saluni na kukuta wanaume wakisafishwa
uso au kufanya scrubing ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikisaidia
kuondoa madoa usoni, mafuta na kufanya ngozi ipendeze.
Unaposafisha uso unaruhusu vitundu vya kutolea hewa kubaki wazi na hivyo
kufanya ngozi kuwa na afya nzuri na hata muonekano wake kuwa bora
zaidi.
Jitahidi kusaifisha uso na kufanyia scub uso wako japo angalau mara
mbili kwa wiki jambo hili kwa kiasi kikubwa husaidia kuondoa seli
zilizokufa kwenye ngozi.
Pia hufanya kuwa laini na ya kuvutia.
Unaweza kupaka loshen au cream za kiume ambazo zipo madukani kwa ajili
ya kuboresha zaidi ngozi yako.
No comments:
Post a Comment