kumekuwa na dhana kwamba uwepo wa vipodozi vya kuondoa mikunjo ya ngozi ni wa miaka ya hivi karibuni, la hasha ukweli ni kwamba krimu za kuondoa mikunjo zilitengenezwa kwa mara ya kwanza huko Misri enzi hizo.
kuna njia rahisi sana ambazo zina uwezo wa kutatua tatizo la mikunjo bila kuhaha katika maduka ya vipodozi kutafuta losheni au vipodozi ili kukabiliana na tatizo hili. Sasa unaweza kutumia vitu vya kawaida kabisa kuondoa mikunjo kwa urahisi na kuufanya uso wako uonekane kijana zaidi. Baadhi ya njia hizi ni kama;
Kutumia tango,yai na limao
- vijiko 2 vya juisi ya matango
- ute mweupe wa yai
- kijiko kimoja cha maji ya limao
Maandalizi:
changanya vitu hivyo kwenye chombo kimoja na hakikisha kwamba vitu vyote vimechanganyika sawasawa. Hifadhi mchanganyiko huo tayari kwa kuupaka kwenye uso.TANGO |
LIMAO |
UTE MWEUPE WA YAI |
Jinsi ya kutumia:
- osha uso wako kwa maji na sabuni na hakikisha umeukausha baada ya kuosha uso wako
- pakaa mchanganyiko wako ulioandaa kwenye uso wako na acha mchanganyiko huo bila kunawa kwa muda wa dkk 15 hadi 20 kabla ya kuosha uso wako
- osha uso wako kwa kutumia maji ya uvuguvugu
No comments:
Post a Comment