Ukiwa mwanaume au mwanamke upigaji sopusopu ni jambo la busara sana ili
kukuweka mtanashati na mwenyekuvutia muda wote kwa kuondoa uchafu na pia
kuondoa mafuta ambayo yana kawaida ya kutanda katika sura.
Kitendo hicho huitwa scrub.Husaidia kuondoa chunusi,vipele na makovu na pia inapunguza mafuta usoni.
Uso
unapokuwa na mafuta sana na kuyaondoa kunasaidia kupunguza vitu vingi
pamoja na vipele na hata mabaka yaliyosababishwa na vipele au chunusi.
Unaweza kutumia scrub ya kwa njia ya mikono kwa kila baada ya siku tatu, na scrub ya mashine baada ya mwezi mmoja.
Scrub
ya mkono.Tafuta aina ya scrub inayokufaa kulingana na ngozi
yako.safisha uso wako mpaka uhakikishe kuwa umetakata kisha chukua scrub
na kuanza kusugua usoni taratibu kwa muda wa dakika tano kisha nawa uso
na unaweza kupakalosheni au poda baada ya kunawa.
Scrub ya mvuke.Chesha maji Nawa uso kwa kutumia maji safi na uhakikishe kuwaumetakata.
Futa uso kwa kutumia taulo safi.
Paka
scrub usoni na pia shingoni kama utapenda. Sugua uso kwa kutoa
taka.Chukua taulo jifunike na kisha inamia beseni lenye maji ya
moto.Baada ya dakika tano toka na subiri kwa muda wa dakika tano
nyingine kisha nawa. Paka poda au losheni.
Pia unaweza kutembelea
saluni za kisasa kwa ajili ya kuufanyia facial uso wako Pia unaweza
kutafuta sabuni ya ukwaju na ukawa unanawa uso asubuhi na jioni hii
huondoa upele, chunusi na mabaka usoni
Saturday, 31 December 2016
NJIA ZA ASILI ZA KUONDOA MIKUNJO USONI.
kumekuwa na dhana kwamba uwepo wa vipodozi vya kuondoa mikunjo ya ngozi ni wa miaka ya hivi karibuni, la hasha ukweli ni kwamba krimu za kuondoa mikunjo zilitengenezwa kwa mara ya kwanza huko Misri enzi hizo.
kuna njia rahisi sana ambazo zina uwezo wa kutatua tatizo la mikunjo bila kuhaha katika maduka ya vipodozi kutafuta losheni au vipodozi ili kukabiliana na tatizo hili. Sasa unaweza kutumia vitu vya kawaida kabisa kuondoa mikunjo kwa urahisi na kuufanya uso wako uonekane kijana zaidi. Baadhi ya njia hizi ni kama;
Kutumia tango,yai na limao
- vijiko 2 vya juisi ya matango
- ute mweupe wa yai
- kijiko kimoja cha maji ya limao
Maandalizi:
changanya vitu hivyo kwenye chombo kimoja na hakikisha kwamba vitu vyote vimechanganyika sawasawa. Hifadhi mchanganyiko huo tayari kwa kuupaka kwenye uso.TANGO |
LIMAO |
UTE MWEUPE WA YAI |
Jinsi ya kutumia:
- osha uso wako kwa maji na sabuni na hakikisha umeukausha baada ya kuosha uso wako
- pakaa mchanganyiko wako ulioandaa kwenye uso wako na acha mchanganyiko huo bila kunawa kwa muda wa dkk 15 hadi 20 kabla ya kuosha uso wako
- osha uso wako kwa kutumia maji ya uvuguvugu
MWANAMKE MREMBO KUKABILIANA NA TATIZO LA KUOTA NDEVU KWA KUFANYA HAYA.
Mwanamke Kabiliana na Tatizo la Kuota Ndevu kwa Kufanya Haya
Wasichana wanapoota ndevu nyingi
hukabiliwa na changamoto za kisaikolojia na ulimbwende. Mitazamo na mila nyingi
za kijamii katika bara la Afrika, bado zinakumbatia unyanyapaa wa wazi au wa
kificho kwa wasichana wanaoota ndevu nyingi. Msichana mwenye ndevu nyingi
anavuta hisia na macho ya wanaume na wanawake wenzake pia kiasi kwamba
anatazamwa kwa namna ambayo wakati mwingine inamnyima raha. Wakati mwingine
wanaume hawapendi kuoa wasichana wenye ndevu nyingi kutokana na mwonekano
unawafanya wasichana hao kuwa kama wanaume.
Katika hali ya kawaida msichana anatazamiwa asiwe na nywele nyingi kwenye kidevu, juu ya mdomo wake, kifuani, tumboni na mgongoni. Na hata akiwa nazo basi ziwe malaika zisizokuwa na rangi nyeusi iliyokolea na kuwa ngumu kama za wanaume.
Mwanamke anapokuwa na nywele nyingi sehemu hizo humaanisha kuwepo kwa hitilafu za kijenetiki au dosari za ulinganifu wa vichocheo vya jinsia mwilini mwake. Wasichana wengine maumbile yao yanayotokana na vinasaba yanawafanya wawe na nywele nyingi mwilini, hali hii kitabibu hujulikana kama ‘hypertrichosis’.Dosari za ulinganifu wa vichocheo vya kijinsia kwa wasichana zinaweza kusababishwa na:-
(1) Kuzalishwa kwa wingi kwa vichocheo vya ujinsia toka katika mifuko ya mayai.
(2) Uvimbe katika mifuko ya mayai (ovarian tumors)
(3) Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango zenye vichocheo pia zinaweza kuwa chanzo cha tatizo hili kwa baadhi ya wasichana. Dawa hizi husababisha ongezeko la vichocheo bandia vya ujinsia kuwa vingi katika mwili wa msichana.
(4) Matumizi ya dawa na vipodozi vyenye viambato vya dawa kama testosterone na steroid zingine pia husababisha tatizo hili endapo dawa hizi zitatumiwa kwa muda mrefu.
(5) Uvimbe wa tezi ya Adrenali iliyo juu ya figo pia unaweza kusababisha tatizo hili.
(6) Unene wa kupindukia (obesity) kwa wasichana pia unaweza kusababisha ongezeko la kichocheo cha kiume (Androgen) mwilini mwa msichana kutokana na nyama zenye mafuta mengi kugeuza kichocheo cha kike cha estrogen kuwa kichocheo cha kiume cha androgen. Androgen inapokuwa nyingi mwilini husababisha msichana kuwa na tabia za kiume ikiwa ni pamoja na kuota ndevu na kuwa na sauti nzito.
(7) Matumizi makubwa na holela ya baadhi ya dawa zenye kemikali kama vile Danazol, Cyclosporin na zingine pia husababisha tatizo hili.Ni vizuri kwa wasichana kuepuka matumizi ya dawa bila kupata ushauri wa kitabibu.
(8) Ikumbukwe kuwa wakati mwingine kunakuwepo na hali ya ulinganifu wa vichocheo vya ujinsia mwilini kama kawaida, lakini tatizo likawa ni mwitikio wa hali ya juu wa nywele (oversensitivity) kwa kiasi cha kawaida cha kichocheo cha kiume kilichoko mwilini mwa msichana (androgen).Katika hali hii, msichana pia anaweza kuwa na nywele nyingi mwilini kuliko kawaida.
Dalili
zinazo ambatana na kuota ndevu kwa msichana
• Kuota chunusi nyingi.
• Kutokupata damu ya hedhi kama kawaida. Wakati mwingine msichana hupata damu pungufu sana, kutoiona kabisa au kupata hedhi yake bila mpangilio maalumu.
• Matatizo mengine yanayosababisha ndevu kuota kwa wingi pia yanaweza kusababisha ugumba (kushindwa kupata ujauzito na kuzaa watoto).
• Kusinyaa kwa matiti na mfuko wa mji wa mimba.
• Kututumuka na kunenepa kwa kinembe kuliko kawaida (enlargement of the clitoris).
• Kuwa na sauti nzito na wakati mwingine kisanduku cha sauti (Adam’s apple) hunenepa kama cha wanaume.
• Mtawanyiko wa nywele mwilini huwa kama wa kiume, pamoja na ndevu msichana huota nywele kifuani, tumboni, mapajani, mgongoni, miguuni na mikononi kwa wingi. Wengine pia huota nywele nyingi kwenye makalio na kuzunguka sehemu ya njia ya haja kubwa na hali hii ya msichana kuwa na nywele nyingi mwilini, hujulikana kama “hirsutism”.

Jinsi msichana anavyoweza kukabiliana na tatizo la ndevu
• Kwanza kabisa msichana anatakiwa
kuelewa kuwa kuota ndevu sio dhambi na wala si kosa, hivyo basi ndevu zisiwe
chanzo cha msongo wa mawazo.• Msichana asiache ndevu zikawa ndefu kama za wanaume kwani zinavuta hisia za watu kumwangalia angalia kiasi kwamba zinaweza kusababisha matatizo ya kisaikolojia. Ndevu zikatwe na kuwa fupi kadri inavyowezekana kwa wakati wote. Mkasi au cream ya kuondoa nywele inaweza kutumika kwa lengo hili. Ile dhana ya wanawake wengi kwamba ndevu zikinyolewa zinaongezeka maradufu haina ukweli wowote wa kisayansi.
• Ni bora wasichana wakajiepusha na matumizi ya vipodozi vyenye viambato vyenye dawa za magonjwa ya ngozi.
• Ndevu zising’olewe kwa vidole, hii inaweza kusababisha uambukizo wa bakteria katika ngozi kwa urahisi na kuleta matatizo ya kiafya.
• Wasichana waepuke matumizi ya dawa zenye steroid bila kupata ushauri wa kitaalamu toka kwa wahudumu wa afya na maswala ya tiba.
• Kufanya mazoezi ya mwili na kudhibiti unene wa mwili pia husaidia katika udhibiti wa tatizo hili.
• Endapo nywele zimetapakaa kwa wingi miguuni na mikononi na kuleta muonekano wa kiume ni bora kuvaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri ili kuepuka msongo wa kisaikolojia ambao unaweza kutokea kutokana na mtazamo hasi wa kijamii.
• Wakati wote jivunie kuwa msichana, usikubali kitu chochote kikuondolee hisia zako za kuwa msichana kamili. Afya ya mwili na roho huanza na afya ya akili. Jitambue, jipende, jiheshimu na jiamini kwani wewe ni msichana kama walivyo wasichana wengine.
RANGI SAHIHI WAKATI WA KUJIREMBA
YAPO mambo mabalimbali katika tasnia ya urembo hasa katika vipodozi yanayopaswa kuzingatiwa katika kuboresha muonekano wa mtu.
Moja ya mambo hayo ni ujuzi na uelewa wa kutumia rangi katika kujipodoa kwani ni wanawake wachache wenye ujuzi huu.
Katika makala hii, nitakuelezea namna ya kuchanganya na kutofautisha rangi za vipodozi, lengo likiwa ni kuboresha muonekano wako.
Uchanganyaji wa rangi za vipodozi ni muhimu sana kwani katika kujipodoa, rangi zote za vipodozi unavyopaka zinatakiwa zioane ili kuleta muonekano ulio sawa na wa kueleweka.
Kwanza kabisa unatakiwa uwe makini katika kuoanisha rangi za vipodozi pamoja na rangi ya ngozi yako, hivyo katika hili unatakiwa kuwa na ujuzi maalumu ili usije ukafanya makosa na kuharibu muonekano wako.
Pia inabidi ufahamu hatua za upakaji vipodozi ili usije ukafanya vipodozi vingine visionekane katika uso wako.
Namna ya kuoanisha na kutofautisha rangi
Siku zote vipodozi vyako lazima viendane na mavazi yako ili kuleta maana zaidi kwa mfano, mara nyingi rangi ya mdomo ‘lipstick’ huendana na vazi lako wakati shedo ‘eye shadow’ zinatofautiana.
Kwa nguo za pinki
Katika mavazi haya, unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya pinki ambayo itaendana sawasawa na mavazi yako huku ukichanganya na shedo ‘eyeshadow’, inaweza kuwa ya rangi ya bluu ili kuitofautisha na mavazi yako, hapo utakuwa sawa katika kanuni za urembo.
Vazi la kijani
katika vazi hili unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya kahawia huku ukichanganya na shedo ya rangi ya kijani au kahawia iliyoingiliana na pinki au rangi ya machungwa.
Kwa vazi la njano au kahawia
Katika vazi hili unatakiwa kupaka ‘lipstick’ ya rangi ya kahawia iliyokolea, kwa upande wa shedo waweza kupaka ya rangi ya dhahabu.
Kwa vazi la bluu
Katika vazi hili unatakiwa kupaka ‘lipstick’ yenye rangi ya pinki huku ukipaka shedo ya rangi ya bluu kwa mtindo huu utakuwa mwenye kuvutia siku zote.
VIPODOZI VIKALI NI HATARI KWA,TUMIA NJIA ASILI
Badala
ya kutumia vipodozi vikali ambavyo wakati mwimgine huweza kusababisha
maradhi kama saratani, ni vyema ukatumia vipodozi asilia ambavyo ni
rafiki wa ngozi yako.
Hata
hivyo aina yoyote ya ngozi ni nzuri hali mradi isiwe na harara, upele
au mabaka. Watu weusi na weupe wasipozifanyia ngozi zao matunzo ni
lazima ziharibike na zipoteze mvuto.
Katika
makala hii, utapata kujua namna ya kuifanya ngozi yako iwe na weupe wa
kipekee kwa kutumia vitu vya asili ambavyo hupatikana jikoni kwako,
tena kwa urahisi.
Haya hapa ni mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kuing’arisha ngozi yako hajalishi uwe na ngozi nyeusi au nyeupe.
Siri ya limao.
Limao linaweza kuufanya uso wako ukapata weupe wa kipekee na kwa wale wenye ngozi nyeusi wakawa waang;avu.
Limao linaweza kuufanya uso wako ukapata weupe wa kipekee na kwa wale wenye ngozi nyeusi wakawa waang;avu.
Kata
limao nusu. Ile nusu nayo ikate nusu, hivyo utapata robo. Sugua limao
katika uso wako na uruhusu juisi yake iingie katika ngozi yako. Baada
ya zoezi hilo acha juisi hiyo ibaki usoni kwa dakika 15. Osha uso wako
kwa maji ya moto. Fanya hivyo angalau mara mbili kwa wiki, na utaona
mabadiliko.
Siri ya asali na maziwa ya unga
Chukua kikombe, weka maziwa ya unga kijiko kimoja, asali kijiko kimoja na juisi ya limao nusu kijiko. Changanya kasha paka usoni na usugue taratibu. Acha ikae usoni kwa dakika 15 na kasha osha taratibu kwa maji ya vuguvugu. Utayaona matokeo baada ya muda mfupi.

Siri ya nyanya na unga wa mahindi
Chukua nyanya moja, isage kasha changanya na unga wa mahindi. Jaribu kuufanya mchanganyiko wako mwepesi ili upakike na ukae usoni. Sugua uso wako kwa mchanganyiko huo na uache ukae usoni kwa dakika 20.

Mchanganyiko wa matunda
Chukua tango, nanasi na papai bichi, visage. Mchangayiko laini utakaopatikana hapo ndiyo dawa yako. Usugue uso wako taratibu kutoka chini yaani kidevuni kwenda juu. Uache ukae usoni kwa dakika 20 kisha osha kwa maji ya baridi

TUMIA MCHANGANYIKO WA ASALI NA PAPAI KUONDOA MADOA USONI.
Kuna maswali mengi yanayoulizwa jinsi ya kuondoa madoa usoni. Lakini jambo kubwa la kuangalia
je madoa uliyonayo
yamesababishwa na nini, Je ni kwa ajili ya kutumia madawa yenye kemikali kali kwa lengo la kupendezesha ngozi au ni
vipele tu vya kawaida.
Wengi wanapenda kutumia sabuni na cream kali ambazo baadaye zimekuwa zilileta madhara makubwa kwenye ngozi zao na
kuwafanya kuwa na mabaka meusi.
Ni muhimu pia kujifunza kutumia vipodozi vya asili ambavyo havina madhara kwenye ngozi.
Unaweza kutumia mchanganyiko wa papai na asali kwa ajili ya kuondoa madoa usoni.
Mchanganyiko huu ambayo huwa laini utauacha ngozi yako ikiwa nyororo na yenye kuvutia.
Namna ya kutumia.
Kwanza ni kusafisha uso kwa maji ya vuguvugu kwa kutumia kitambaa laini pia unaweza kusafisha hadi shingoni na hakikisha
uso umekataka kisha futa uso wako na shingo kwa taulo.
Andaa asali yako pembeni kisha kata papai na kisha liponde hadi kulainika kabuisa.
Baada ya hapo changanya rojo hiyo ya papai na asali koroga hadi kuhakikisha umepata mchanganyiko mzuri.
Anza kupata usoni taratibu hadi maeneo ya shingo unaweza kukaa na mchanganyiko huo kwa robo saa kisha safisha uso
wako.
Unaweza kutumia mchanganyiko huu mara kadhaa kwa wiki mpaka upate matokeo mazuri kwenye ngozi yako.
Lakini jambo la msingi ni kuhakikisha anaepuka kutumia cream zenye kemikali kali kwani zimekuwa na madhara kwenye
ngozi.

Wednesday, 28 December 2016
JINSI YA KUPAKA MAKE UP USONI.
Sasa leo nimekuja na TIPS chanche za kukufanya wewe uonekane mrembo zaidi kila wakati .
1. USO -
osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu na sabuni. kausha vzuri na kitaulo laini.
kama unatumia cleanser yoyote ni vizuri zaidi kuondoa uchafu kwenye uso
wako kwa kutumia pamba na baada ya hapo osha tena uso wako kwa maji tuu
ya uvuguvugu na ujikaushe.
2. FOUNDATION
Chagua faoundation inayoendana na rangi ya ngozi yako,
foundation ndo ya kwanza
kupaka usoni kwako ili kuziba vidoa doa vilivyo kwenye ngozi ya uso wako
,paka kwa kutumia brush maalum ukianzia katikati kwenda chini na
juu.epuka kuanzia kwenye pji la uso yani nywele zinapoanzia kwani
itasbabisha mlundikano.
3. POWDER
Paka powder inayoendana
na ngozi yako juu ya foundation,hakikisha unasambaza uso wako wote
pamoja na sehemu za shingo ili rangi iwe sawa na uso. kwa kutumia
spounge au brush inayohusika.
NB: ZINGATIA SANA RANGI YA PODA PAMOJA NA RANGI YA NGOZI YAKO ,KWANI UNAWEZA UKAWA MNG'AVU THEN UKAPAKA PODA AMBAYO ITAKUFIFIZA
UREMBO WA NYUSI / EYE BROWS SHAPING
Urembo: Nyusi
kwa kawaida shape ya nyusi inategemea na sura ya mlengwa
lkn pia kuna vipimo ambavyo vitakusaidia wakati wa kutinda nyusi zako na kupaka wanja.
fatilia picha zifuatazo
Nyusi ina sehemu kuu tatu kama zilivyoonyeshwa hapo juu..
1. Inner Corner
ambayo inakutanisha mwanzo wa jicho na mwanzo wa nyusi unatakiwa utengeneze nyuzi 90(mstari unyooke kukutanisha hizo corner.
katika angle hii nusi inatakiwa iwe nene kuja kwenye high point
2. High Point
Hii ni sehemu special kwa ajili ya kuigawa nyusi na nisehemu ya mkunjo kutenganisha inner corner na outer corner.
na pia unaanza kuichonga kwa kuipunguza unene.
3. Outer Corner
angle hii inakutanisha mwisho wa nyusi na mwisho wa jicho lenyewe kwa mstari ulionyooka kuifata hii corner.
Hapa ndipo huwa pembamba kutokana na mchongo mzima.
NB: Hizi lines zote zinaanzia kwenye angle ya pua kama mchoro huu
Baada ya kushape vizuri nyusi zako kutokana na michoro hapo juu.
mchoro huu utakuongoza vizuri jinsi ya kupaka wanja kwenye nyusi zako.

UREMBO NA LAURA:...
JINSI YA KUPAKA WANJA MNENE a.k.a WANJA WA LULU
Asalam Aleykum wasomaji wangu!
Leo nakuletea tena lile somo la kupaka wanja mnene a.k.a wanja wa Lulu!
Tuelewane kwanza....huu wanja waaaala hauchagui, uwe na nyusi msitu uwe
na nyusi za kuokoteza, dada kwa wanja huu wote mtafanana na kupendeza!
wanja huu haujawahi kumchukiza mtu!
Pili, uwe na wanja wa pencil au wanja wa poda wote mnaweza kuuchora huu
wanja. Sasa wenzangu na mimi mnaoona ubahili wa kununua wanja wa elfu 20
ule poda usijisikie unyonge. Huu niliojipaka hapo pichani ni wa elfu
mbili tu hahahhaaa shame on me!
Tatu, Wanja huu hautaki mkata tamaa kwenye kujifunza...weka nia tu kuwa
mara mbili tatu nitaweza maana kuna akina dada mnajidekeza bwana aah mi
siwezi... aah mi siwezi nitakufuata uko na bakora nikucharaze viboko
mpaka uweze...usinitanie! hahahahaaaa
Anyway, hebu tuanze somo letu....
Watu wengi huuliza unatumia vifaa gani kuuchora?.... hapa nitakuwekea
vifaa ambavyo mara nyingi hutumika haswa na sisi tunaojitengeneza
wenyewe majumbani.... wale wa saluni uko kuna brands za vifaa na
vipodozi... ila simple tu ya kama yangu hiyo aaah ndugu yangu vifaa vya
malaki havinihusu!
TAFADHALI SOMA MAELEZO VIZURI USIPOELEWA RUDIA!! au ULIZA!...ULIZA!!
...ULIZA!!
A. MAHITAJI
1. UNAHITAJI WANJA
Wanja wa pencil uwe Black au Brown
hapa nakushauri nunua wanja mkavu uwe mgumu kidogo
Wanja wa Poda uwe Black au Brown
Huu hapa chini ni wa kwangu.
Huu wangu uko double. Upande mweusi ni wanja
upande huo mwingine ni Concealer (nitaelezea kazi yake chini uko)
2. UNAHITAJI BRUSH MOJAWAPO KATI YA HIZI...
Nasisitiza moja wapo au ukiwa nazo zote sio mbaya pia!
Hizi za chini ni zangu.... ninazo zote!
The funniest Part is nilitafuta brush kama hiyo ya kulia nikakosa
ikatokea tu mtu akataka kuniuzia kwa bei ya nauli Dar to Mwanza
hahahahaaa
Nikaona tabu ya nini...nikanunua Mascara tu duka la urembo nikachomoa
hicho kidude
nikakioshaaa baaasi nikatimiza haja ya moyo!!
3. UNAHITAJI CONCEALER...
Zipo Concealer za muundo tofauti na rangi tofauti.... utachagua muundo
wowote upendao cha muhimu...narudia cha muhimu...chukua concealer
inayoendana na rangi yako!
Zipo hizi kama Pencil...usichanganye na wanja huu sio wanja
Na ndio kule juu kwenye wanja wangu kuna concealer pia, yaani two in
one!
kuna hizi zimekaa kama lipstick hivi....
kuna aina hii ya kwenye kikopo
Hii hapa chini ndio yangu sasa...!!
4. UNAHITAJI CHA KUPAKIA CONCEALER...
kuna watu wanatumia vidole lakini concealer haitachonga vizuri kingo za
wanja wako ukitumia vidole. unahitaji kibrush chake hasa kama unatumia
concealer ya kikopo kama hiyo yangu. hizo concealer za pencil au ctick
unaweza kuchorea tu bila kuhitaji brush kivile... Umeelewa?
Brush yangu ndio hiyo....
B. NAMNA YA KUUCHORA SASA....
Ukishakuwa mjuzi hutaitaji kanuni hizi zinazoanza nazo hapa...yaani '
automatically' utajichora fasta tu bila kufuata vijikanuni...ila wewe
unayejifunza nitakupa hizi kanuni mbili. Ili uelewe vizuri. So usidhani
utazifuata kila siku.... hapana zitumie unapojifunza basi, ukishakuwa
mzoefu wala hutohitaji!
1. KANUNI YA KWANZA...
Hii ndio kanuni ya kwanza....
Unapaswa kujua wanja wako unauchora kuanzia wapi?
Utauinulia wapi?
na utaishia wapi?
Kanuni hii itakusaidia kuchora nyusi zinazofanana
Sio nyusi moja imeinuka mwishoni mwa jicho uko nyingine imeinukia
katikati
Utachekesha umati wa Mtume Wallah! hahahahahaaaa
Tumia kitana au chochote tu kupimia.... na pia hapo palipo inuka kidogo
ni uamuzi wako painuke sana au painuke kidogo ni wewe tu mchoraji...
Umeelewa sasa?
2. KANUNI YA PILI....
Chora mstari hivi....
Halafu chorea juu upate kitu kama hiki
Si unaona kwa juu kainua ndio kanuni ya kwanza ilipotumika
Sasa wewe utainua kwa kiwango unachopenda wewe juu zaidi au hivi hivi
Yote kheir!!
Tumemalizana na Kanuni... sasa umeshachora hicho kimchoro... twende
hatua ya pili
---- Anza kujaza wanja kwenye nafasi katikati ya mchoro wako...
usikandike shoga fanya kupaka juu juu. Ujanja hapa ni anzia kujaza
mwisho mpaka katikati hivi... huku mwanzoni mwa nyusi utapajazia na
kibrush ili pawe pepesi hivi...
---- ukishajaza jaza chukua kibrashi kimojawapo...anza kuparaza nyusi
sasa... sawazisha kule nyuma kisha rudi huku mbele napo paraza
vizuri.... sababu umeanzia mwisho basi brashi itakuwa imepata wanja so
ukiparaza patajaa tu... ukipenda unaweza kutumia wanja wa brown kujazia
mbele napo inasaidia kuleta wepesi.
---- Paraza mpaka uone umeenea vizuri na huku mwanzo pamekaa vyema....
paka concealer yako
Concealer yako itachonga vizuri kingo za nyusi zako
Kama hivi!...sasa kazi ya kibrush cha concealer ndio hii kunyoosha nyusi
zako!
unaona Concealer inavyoshepu nyusi zako
Umeona hapo?....
Concealer ina kazi nyingine ya kuficha alama nyeusi usoni
Hiyo sitoizungumzia leo.
Leo ni kujua namna ya kushepu nyusi
NIMEJICHORA MWENYEWE SASA
Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef

NAMNA YA KUBORESHA MAKALIO
Wanawake wengi kwa
sasa wanakwenda kuboresha makalio yao ili kuyapatia ukubwa unaostahili kwa
jinsi wao wanavyopenda.
Tatizo hili halipo
hapa nchini lakini wapo walionituipia swali sasa inabidi nikiri kuwa lipo sana
marekani na mpasuaji wa masuala ya urembo wa Miani Dk Costantino Mendieta
amethibitisha.
Katika fasihi yake
mtaalam huyo amezungumzia sana utunzaji wa makalio kwa kuyagawa katika madaraja
manne.
Anasema makalio
daraja la kwanza ndiyo yanayotakiwa sana > Ni kama vile umechukua moyo
halafu ukaugeuza chini juu haya ndiyo dizaini ambayo Marekani wanalilia sana.
Watu wa huko wanajimwaga katika majumba ya upasuaji kupata shepu hiyo adimu.
Hatua hizo ni kama ifuatavyo.
1.fanya masaji na
losheni zinazoimarisha na kutengeneza ngozi mwororo katika mapaja yako ukianzia
chini ya makalio mara mbili kwa siku.
2.Ondoa miinuko
midogo midogo isiyotakiwa ni yako kwa kuskrabu mara mbili au tatu kwa wiki
ukitumia salt scrub.
3.Pamoja na
matatizo ya michuchumio, ivae ili kukupa nafasi ya kutembea kwa miondoko ya
twiga inayotoa nafasi nzuri kwa makalio kuwa na mvuto.
4.tafuta namna
nzuri ya kuficha michirizi ya kunyooka kwa misuli ya mwili.
5.Mazoezi
yatakufanya uwe mtu tofauti zaidi pandisha ngazi kwa dakika kumi au zaidi na
chukua mazoezi ya kubana makalio yako na sehemu za kiuno kwa kusukuma kwa ndani
na kutulia hivyo kwa sekunde tano na kujiachia na unaweza kufanya hivyo
unavyotaka.
Pia unaweza
kuongeza uzuri wa makalio yako kwa kuhakikisha unakula vyema na unakula
inavyostahili.
MWANAUME KUWA NA NGOZ NZURI HULETA FURAHA,KUJIAMINI..
UMARIDADI WA KUPAKA KUCHA RANGI.
Ili uwe na kucha maridadi masuala ya kuzisafi na kuziweka rangi ni muhimu ama sivyo? na kwa kawaida kucha zilizo safi ndizo hasa zinazokubali polishi yaani rangi au sivyo?
Na ama hakika kucha zilizo safi ndizo hasa zinazotengenezwa na kuwekwa sopusopu.
Ni vyema kutambua kwamba wakati wa kupaka rangi tumia mipako michache kwa kila mpako na kila mpako uachie ukauke kabla ya kuanza mpako mwingine.
Na ile ya mwisho inatakiwa kuwa bomba zaidi kwa kuwa ndio hasa itakayokuwa inatunza matabaka mengine yote.
Utengenezaji mzuri wa kucha si lazima uwe wa kwenda katika mapumziko au kuonyesha mtu ni kitu ambacho kinafaa kufanywa ili uwe mrembo kila mahali.
Kuna raha ya kujisikia katika rangi mpya katika mwaka mzima na hasa kama uchaguzi wako wa rangi za kupaka ni bomba.
Moja rangi ya pinki ama nyekundu inakupa nafasi ya kuwa funny . Unaweza kujipaka rangi mwenyewe au kuwambia mtu akupake rangi.Kuna hatua kadhaa ambazo unatakiwa kuzifanya kabla ya kupaka rangi kucha zako.
Hatua ya kwanza ni kuondoa rangi zote za awali.kwa kufanya hivyo rangi mpya itakuwa ina uwezo wa kushika katika kucha.
Pia kunasaidia rangi yako mpya isitibuliwe na rangi ya zamani kwa namna yoyote ile.
Unaweza kuondoa rangi ya zamani kwa kutumia dawa inayopatikana katika maduka ya dawa na hata yale ya vipodozi na pamba hufanya vyema kartika kuondoa rangi za kucha kwa kutumia Nail polish remover.
kazi ya pili ni kutafuta rangi inayokupendeza. unaweza kutumia rangi yoyote kwa sababu mara nyingi viatu vinazuia kuonekana kwa kucha zako la kama unahitaji rangi fulani kwa sababu miguu yako i wazi ni vyema sana.
Tazama kwamba vipaka rangi vyenyewe ni vipya kwani vilivyozeeka huleta tatizo kidogo.mara nyingi vipaka rangi vilivyokaa miaka miwili havifai tena kutumika.
Anza kupaka baada ya kubainisha kwamba unaweza kutenganisha kidole kwa kidole ili usipake kila mahali hasa kama brashi husika ni pana kidogo.
Anza katikati kwa kuanzia nyuma kupeleka mbele kisha nenda pembeni na pembeni.Na baada ya kukauka unaweza kuongeza tabaka jingine tena na tena.
Kisha paka ile ya mwisho ambayo ndiyo italinda rangi yenyewe yaani top coat . top coat husaidia sana kuweka rangi kwa muda mrefu. Top coat ni polishi isiyokuwa na rangi na kama unataka kuweka stika iweke mapema kabla ya kuweka top coat.
rangi nzuri na zilizotulia zinakufanya uwe na sababu ya kujivalia sandals zako nzuri au viatu vya wazi
UMUHIMU WA MANUKATO KATIKA UREMBO WAKO.
Ukitaka kuwa mrembo ni wazi kuwa unatakiwa kuuweka mwili wako katika hali nzuri ya kupendeza kuanzia mavazi, mitindo ya nywele.Ndio kusema kuna vikorombwezo kibao vinavyotakiwa ili kukufanya uwe mrembo zaidi.
Manukato nayo ni muhimu katika kunogesha urembo wako.Nadhani ulishawahi kusifiwa au kusifia mtu kutokana na manukao anayotumia na wengi wetu tumekuwa tukitumia aina za manukato ambazo tunaona zinatufaa zaidi.
Ni vizuri kuchagua aina ya manukato na njia nzuri ni kupulizia kigogo kwenye mkono wako ili uweze kujua harufu yake kama umependezwa nayo au laa. Usitumie manukato ya aina fulani kwa sababu fulani anatumia.
Jaribu kutafuta aina ya manukato uliyoyachagua kwani kuwa mnukato yana harufu kali na hili huleta taabu kidogo kwa baadhi ya watu unaokuwanao karibu.
Chagua manukato ambayo yana harufu iliyotulia na pia ukali wa manukato wakati mwingine husababisha kujipulizia kiasi kikubwa cha manukato hali ambayo huwa kero kwa wengine.
Jaribu kutumia manukato kiasi fulani kwani aina nyingine hudumu muda mrefu na unapojipulizia manukato ona unafanya hivyo kwa faida yako na sio kuhakikisha kuwa kila mtu anajua umetumia manukato ya aina fulani hapo ndiyo huleta shida kidogo kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha manukato na hivyo kuleta shida kwa wengine.
Pia unashauriwa kutotumia manukato ili kuondoa harufu ya mwili kutokana na kutooga au kutokana na sababu nyingine hapo maana ya manukato hupotea. Manukato hupendeza iwapo yatapuliziwa wakati mwili na nguo zikiwa safi. Tumia aina ya manukato uipendayo ili kuweza kukuweka mrembo zaidi.
UVAAJI WA BANGILI NA MAANA ZAKE.
BANGILI ni kitu kilichotengenezwa kwa lengo la kuvaliwa mkononi kama saa.
Bangili hutengenezwa kwa kutumia ngozi, kitambaa kigumu, plastiki, chuma, na wakati mwingine huwa na nakshi za aina mbalimbali.
Fasheni za bangili hutegemea na matakwa ya mavaaji kwani kuna wale ambao wanapenda kuvaa bangili zilizotengenezwa kwa vito vya thamani kama dhahabu na almasi na wengine wakipendelea kuvaa bangili zilizotengenezwa kutokana na vitu vya asili.
Bangili licha ya kuwa ni urembo wa mkononi, wakati mwingine hutumika kama alama hasa kwa wagonjwa wanapokuwa hospitalini na hutumika kama alama ya mgonjwa.
Hapa nchini kumekuwa na wasanii wa uchongaji ambao
hutengeneza bangili kwa kutumia magome ya miti na wakati mwingine kwa kutumia vifuu vya nazi.
Inaaminika kuwa bangili ambazo hutokana na vifuu vya nazi zimekuwa zikipendeza kuvaliwa kutokana na muonekano wake kwa ujumla na pia huuzwa kwa gharama nafuu ambapo wengi wanamudu kununua kuliko bangili zilizotengenezwa kwa vito vya thamani.
Uvaaji wa bangili pia unatakiwa kuzingatia rangi ya mvaaji, kama mtu ni mweusi anashauriwa kuvaa bangili zenye mng'ao ili kuweza kuwa na muonekano mzuri.
Ni vizuri kama tutazingatia mpangilio wa rangi katika uvaaji wa bangili na itapendeza kama uvaaji huo utazingatia na rangi ya nguo au viatu.
UREMBO WA MACHO UTAKUFANYA UONEKANE MREMBO ZAIDI.
Eyeshadows ni urembo ambao hutumiwa juu na chini ya kope. Njia hii husaidia kuongeza kina na mwelekeo wa macho ya watu.
Watu wanapenda kutumia aina hii ya urembo ili kuweza kuimarisha muonekano wao.
Kama wewe ni mweusi jaribu kutumia rangi angavu ili kuimarisha muonekano wako ukitumia rangi za giza zitakufanya uonekane vibaya.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa unakuwa makini ili kuweza kuweka macho yako katika hali bora zaidi ya kupendeza.
Wakati mwingine Eyeshadows hufanya macho kuonekana makubwa au madogo. Lakini cha muhimu kuzingatia je rangi unayopaka inaendana na macho yako au ngozi yako.
Unatakiwa kupaka rangi kwa ustadi mkubwa huku ukiweka mkolozo katika kona za macho yako.
Ni vizuri kama utatumia eyeshadow ya penseli kwani huwa rahisi kuitumia na inapatikana kwa urahisi madukani.Kuna rangi za aina nyingi ambazo hupendeza wapakaji, rangi hizo ni pamoja na pink plum, matumbawe na shaba, bluu na kijani
pamoja na fedha, dhahabu na nyingine nyingi.
Rangi hizi hutofautiana kulingana na mng'ao wake kwani kuwa zenye mng'ao mkubwa na zile zilizofifia.Njia ya kawaida ya kupaka eyeshadow ni kutoka ndani ya kona
ya jicho na nje na zaidi.Rangi kama Gray, violet, zambarau na bluu huwapendeza sana
watu wa rangi ya maji ya kunde na kusaidia kung'arisha macho yao.
MIKOBA INAVYOCHANGIA UREMBO KWA WANAWAKE.
UNAPOKUWA katika safari zako utaona jinsi wanawake wanavyobeba mikoba ya aina mbalimbali.
Wakati mwingine mingi ya mikoba huwachukiza na wengine huwa kichekesho na ingawa wengine urembo wao huambatanishwa na kujipachika tu, vitu maarufu kama vipima joto kwa lugha ya kileo.
Ukiangalia hasa mijini hakuna kabati la nguo la mwanamke ambalo litakosa mikoba, tena ya aina mbalimbali. Kwa mwanamke kuwa na mkoba moja si sawasawa, kwa wale wanaokwenda na wakati kuwa na aina nyingi ya mikoba hii hutokana na ukweli kuwa mikoba hiyo ni sehemu ya mavazi na huambatana na si tu aina ya pamba iliyopigwa bali aina ya viatu vinavyompa kampani mwanamke.
Mwanamke ni kiumbe mrembo kabisa na jinsi anavyozidi kumechisha vitu anatakiwa kuwa mrembo na mwangalifu zaidi kwani anahitaji kujiweka katika kiwango kinachostahili katika kazi zake na uonekano wake.
“Mavazi yako unayovaa yanaweza kabisa kubadili maisha yako” anasema Trinny Woodall mmoja ya watu ambao wako makini kabisa na masuala ya unadhifu wa wanawake wa wanawake katika mitoko ya aina mbalimbali aliyeko Afrika Kusini.
Inakuwaje unapokuwa na vazi tofauti na mkoba wako wa kwapani na ndiyo huo mkoba mmoja pekee unaotumia kwa kwenda pati, kwenda safari. Kwenda kazini na kadhalika?
Hakika kwa mwanamke anayejijali, anatakiwa kuwa na mikoba ya aina tofauti kwa kuzingatia haja ya shughuli zake na pia mavazi yake.
Unachotakiwa siku zote si tu kuwa na mikoba mingio, najua unaweza kuwa na mikoba, unaoupenda lakini ni dhahiri kwamba mikoba hiyo unatakiwa lakini ni dhahiri kwamba mikoba huyo inatakiwa kuwa na mwendo sawa na mavazi yako ili kukupa kitu bomba kinachoweza kuwafanya wanaume wakutazame mara mbili mbili na wanawake wenzako wakuonee gere.
Nina sababu ya kukuambia hivyo lakini wapo wanawake waliojaza mikoba kibao lakini hawaitumii lakini hapo mwanzao waliponunua walijua kwamba ni mikoba bomba kabisa yenye mvuto wa kimapenzi hasa.
Kitu cha kwanza kuzuia ni ule ufujaji wa kununua mabegi yasiyotakiwa, yaani ni kuwa makini na haja yako mwenyewe na mapenzi yako na namna wewe mwenyewe ulivyo.
Ndiyo kusema mkoba lazima uzinagatie mwili wako, upenzi wa maisha yako.
Watengeneza mikoba wengi wanaonya kabisa uchukuaji wa mikoba kwa kuiona bomba kumbe hairandani na wewe unayeibeba.
Mathalani wewe ni mrefu na mwembamba, mikoba yenye mduara ni mizuri lakini kama wewe ni mfupi uliyejazia kiasi chake mkoba unaofanana na ule wa mstatili, mrefu kiasi na mweroro ni kiboko yake.
Ningekushauri kabla hujanunua na kuvaa mikoba hiyo hebu jitazame kwanza katika kioo kwani ni lazima ukubali kwamba uko safi ndiyo uchangamke na mtaa, unapokuwa umejiangalia kwenye kioo utapata namna bora namna bora ya muonekano kama vile unavyojaribu nguo kwenye kioo.
Mikoba myembamba iliyobana hasa huonekana kuwa bomba kwao kama wewe ni mwembamba pia na kama unataka mtu kujisahau kwa namna yake katika mwili wako, lakini haitakusaidia sana kwa matiti yako ni madogo na mikono yako haijajaza inavyostahili.
Halafu tazama sana mikanda ya mikoba ina maana kubwa zaidi ni ndiyo maana ni vyema ikazingatiwa urefu wake katika mabega yako kwani kwa vyovyote vile urefu wake utakavyobeba mkoba wako ina kitu inakifanya katika mwisho wake.
Kwa hiyo kama hutaki mushkeri katika maeneo ya juu ya mapaja usitwae mkoba unaofika pale. Wengi wa wanawake hutokea bomba kama mkoba haufiki katika kiuno au juu yake kidogo, kwani kuketi hapo chini inakuwa mambo si poa katikati ya mwili kwa upande wa juu ndiyo haswaa sawa.
Ni muhimu ukitambua ya kwamba ukubwa wa mkoba wako unaambatana na wewe unaeleweka.
Lakini niseme moja tu mikoba mingi huwa bomba kama haijazwi vitu lakini mathalani kama una simu, shajara na vikorombwezo vya uzuri mkoba mwembamba haufai kwani utatuna na kuchukiza.
Mbunifu wa FUNEKA, Tasleem Bulbulia anasema kwamba mtu wa aina hii kwa kulingana na kazi zake na stahili zake za maisha mikoba mipana ni saizi yake. Ndiyo kusema kazi na stahili yako ndiyo pia itazingatia aina ya mkoba unaotakiwa kuwa nao.
Ulishatambua personaliti yako na aina yako ya maisha ni vyema ukatambua ukweli kuwa chagua kulingana na wewe na si yule kwani kivigezo haiwezekani na kwa maisha pia haiwezekani.
mwisho
TUWE WAANGALIFU NA KUCHA ZA BANDIA.
UNATUNZAJE MIKONO YAKO?
Watu wengi wamekuwa wakitengeneza nyuso zao na kusahau kabisa habari za kutunza mikono kitu ambacho si sawa sawa.
Unatakiwa kujifunza vitu gani vinatakiwa ili kuweza kuiweka mikono yako katika hali nzuri ikiwemo aina ya scrub na moisturizer ambayo itafanya mikono yako kuwa katika hali nzuri kila wakati.
Unaweza kutengeneza mikono yako ukiwa nyumbani au hata saluni lakini kama utafanya mara moja kwa wiki utakuwa na mikono ambayo iinaonekana vizuri.
Ili kutengeneza mikono yako unatakiwa kuwa na nail file (tupa ya kucha), brashi ya mikono, kitu cha kukatia kucha (hata webe unafaa) losheni ya mikono, taulo sabuni na maji wa vuguvugu.
Unatakiwa kuosha mikono na ukate kucha na kisha anza kuzisugua taratibu kwa kutimua tupa.
Kisha weka maji ya vuguvugu kwenye beseni na tumbukiza mikono kaa kwa muda wa dakika tano ili kuwezesha ngozi ya mikono kulainika.
Kisha anza kusugua mikono taratibu unaweza kutumia kitambaa laini ila unachotakiwa kuhakikisha unasafisha hadi sehemu za katikati ya vidole baada ya hapo suuza mikono yako na ufute kwa taulo halafu paka lotion ya mikono. Njia nzuri pia ya kutunza mikono ni kuhakikisha unakula chakula chenye kulainisha mwili na kunywa maji mengi.
Kama unakuwa hujali mwili wako na hunywi maji mengi unaweza kuwa na mikono mikavu.
Tuesday, 27 December 2016
JINSI YA KUPAKA MAKE UP USONI.
Sasa leo nimekuja na TIPS chanche za kukufanya wewe uonekane mrembo zaidi kila wakati .
1. USO -
osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu na sabuni. kausha vzuri na kitaulo laini.
kama unatumia cleanser yoyote ni vizuri zaidi
kuondoa uchafu kwenye uso wako kwa kutumia pamba na baada ya hapo osha
tena uso wako kwa maji tuu ya uvuguvugu na ujikaushe.
2. FOUNDATION
Chagua faoundation inayoendana na rangi ya ngozi yako,
foundation
ndo ya kwanza kupaka usoni kwako ili kuziba vidoa doa vilivyo kwenye
ngozi ya uso wako ,paka kwa kutumia brush maalum ukianzia katikati
kwenda chini na juu.epuka kuanzia kwenye pji la uso yani nywele
zinapoanzia kwani itasbabisha mlundikano.
3. POWDER
Paka powder inayoendana na ngozi yako juu ya foundation,hakikisha unasambaza uso wako wote pamoja na sehemu za shingo ili rangi iwe sawa na uso. kwa kutumia spounge au brush inayohusika.
3. POWDER
Paka powder inayoendana na ngozi yako juu ya foundation,hakikisha unasambaza uso wako wote pamoja na sehemu za shingo ili rangi iwe sawa na uso. kwa kutumia spounge au brush inayohusika.
4MACHO
.uso wako ukiwa tayari ,andaa vifaa kwa ajili ya macho yako na nysi zako ambazo zitakua tayari zimechongwa vizuri,hapa inahitajika wanja brown/ mweusi ,eyeliner na eye shadows chagua rangi ianyoendana na ngozi yako au inayoendana na nguo utakazovaa ili kuleta maana.

chora
vizuri nyusi zako kwa wanja wa brown , na upake eyeliner juu ya kope
zako ili kuzipa rangi,then ndo unakuja kuweka eyeshadows ,ni vizuri
kupaka eyeshadow za unga kuliko za maji .yani namaanisha kavu au za
vumbi.
5.LIPS
kama ni mpenzi wa lipstic za mafuta anza kwa
kupaka lipshine ili uweze kulainisha lips zako then paka lipstick yako
kulingana na rangi ulioichagua then paka na lipliner pembezoni mwa lips
zako ili kuwekea ukingo.na kama ni mpenzi wa lipstick kavu haina haja ya
kupaka lipshine paka lipliner yako then paka lipstick yako rangi
uipendayo .
LIPSTICK KAVU . |
Baada ya kufuata hatua hizo tano hapo juu mdau wangu utakua tayari kwa mtoko wako .
ZINGATIO
Katika upakaji wa foundation na Powder
unatakiwa uzingatie mda sababu kuna foundation nyingine ni kwa ajili ya
mchana na nyingine ni kwaajili ya mitoko ya usiku hivyo basi ni muhimu
kuzingatia na kuwa na make up ya mchana na ya usiku kuepuka
mchanganyiko.
NB baada ya kumaliza shughuli zako hakikisha
hulali na makeup yani wakati wa kulala hakikisha unanawa uso wako
vizuri au unaweza futa kwa kutumia make up remova
Ngozi zenye mafuta na jinsi ya kuzitunza
Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.
Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:
• Kuridhi.
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya unyevu (humidity) na hali ya hewa ya joto.
Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta
Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.
2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipotze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.
4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.
5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.
6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.
7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.
8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.
9. Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.
UREMBO NA USAFI: JIFUNZE JINSI YA KUONDOA WEUSI KWENYE SHINGO BILA KUTUMIA KEMIKALI
Kuwa na shingo nyeusi ni malalamiko ya kawaida ambapo kuna sababu chache
ambazo zinasababisha tatizo hili. Moja ni kutosafisha vizuri shingo
yako kwa kuwa na tabia ya kupuuza shingo wakati kusafisha na kuscrub
uso.
Wakati mwingine, hii inasababishwa kwa kuwa na mkusanyiko wa uchafu ambao hufanya ngozi shingoni kuwa nyeusi nakukosa mvuto.
Sababu nyingine ni kwamba shingo ina mikunjo kadhaa ambayo ngozi huwa
inahifanyi vumbi na chembe jasho shingoni ambapo baada ya muda
husababisha ngozi ya shingoni kuwa na weusi. Kutokana na sababu hizi
inakupasa kuwa makini unaposafisha mwili wako hasa sehemu hii ya
shingoni.
Ili kuweza kuongoa weusi huu kila siku hakikisha unasafisha ngozi yako ya shingo na kuondoa ngozi iliyokufa kwenye shingo angalau wiki mbili kabla ya kuona matokeo.
Ili kuweza kuongoa weusi huu kila siku hakikisha unasafisha ngozi yako ya shingo na kuondoa ngozi iliyokufa kwenye shingo angalau wiki mbili kabla ya kuona matokeo.
- Tumia maziwa plain kusafisha shingo yako. Maziwa ni cleanser nzuri na vile vile toner nzuri. Baada ya kusafisha, scrub shingo yako na scrub yenye chenga chenga ili kuondoa ngozi iliyokufa. Unaweza kutumia Scrub yoyote kwa ajili ya kuondoa dead skin kwenye shingo yako.
- Lakini kama hutaki kuwekeza katika moja, unaweza pia kutengeza scrub yako mwenyewe. Unaweza kufanya mchanganyiko wa wa mafuta ya Olive na Sukari kwa kutumia hii scrub shingo yako hii paka kwenye shingo yako pole pole kwa mviringo mpaka sukari iyeyuke yote. Scrub hii itasaidia na hata kuleta tone kwenye ngozi yako.
- Pia unaweza kufanya mchanganyiko wa walnuts na maziwa ya mtindi na pia ongeza matone kadhaa ya maji ya limau na kisha massage mchanganyoko huu kwenye ngozi yako hatua kwa hatua na taratibu.Kukumbuka kwamba hii ni kidogo abrasive, ukizingatia kuwa walnuts si kama sukari haziwezi kuyeyuka na unatakiwa unapopaka mchanganyiko huu usutumie nguvu maana unaweza ukajiumiza.
- Pia kuna baadhi ya matukio machache na ya kawaida ambayo kwa rangi ya asili ni sehemu ya tatizo. Ufanisi zaidi wa asili ya ngozi unatakiwa huduma ya dawa kwa ajili ya kesi ya rangi ya asili ni kutumia Aloe Vera Gel kwa eneo lenye weusi shingoni mwako. Unaweza kupaka na kuacha Aloe Vera Gel kwenye ngozi yako mara nyingi kama inawezekana.
- Kupaka maji ya limau shingo pia itasaidia kuondoa weusi kwenye shingo kwa kiasi fulani. Lakini kumbuka kufanya hivyo usiku tu, hivyo kwamba huwezi kwenda nje katika jua na mabaki ya maji ya limau kwenye shingo yako. Kama utatoka ukiwa umepaka maji ya limau kwenye shingo wakati wa jua itasababisha ngozi yako kuwa nyeusi.
Subscribe to:
Posts (Atom)