wittybeautynews
Thursday, 9 February 2017
Saturday, 31 December 2016
NAMNA YA KUONDOA VIPELE NA MAFUTA USONI.
Ukiwa mwanaume au mwanamke upigaji sopusopu ni jambo la busara sana ili
kukuweka mtanashati na mwenyekuvutia muda wote kwa kuondoa uchafu na pia
kuondoa mafuta ambayo yana kawaida ya kutanda katika sura.
Kitendo hicho huitwa scrub.Husaidia kuondoa chunusi,vipele na makovu na pia inapunguza mafuta usoni.
Uso unapokuwa na mafuta sana na kuyaondoa kunasaidia kupunguza vitu vingi pamoja na vipele na hata mabaka yaliyosababishwa na vipele au chunusi.
Unaweza kutumia scrub ya kwa njia ya mikono kwa kila baada ya siku tatu, na scrub ya mashine baada ya mwezi mmoja.
Scrub ya mkono.Tafuta aina ya scrub inayokufaa kulingana na ngozi yako.safisha uso wako mpaka uhakikishe kuwa umetakata kisha chukua scrub na kuanza kusugua usoni taratibu kwa muda wa dakika tano kisha nawa uso na unaweza kupakalosheni au poda baada ya kunawa.
Scrub ya mvuke.Chesha maji Nawa uso kwa kutumia maji safi na uhakikishe kuwaumetakata.
Futa uso kwa kutumia taulo safi.
Paka scrub usoni na pia shingoni kama utapenda. Sugua uso kwa kutoa taka.Chukua taulo jifunike na kisha inamia beseni lenye maji ya moto.Baada ya dakika tano toka na subiri kwa muda wa dakika tano nyingine kisha nawa. Paka poda au losheni.
Pia unaweza kutembelea saluni za kisasa kwa ajili ya kuufanyia facial uso wako Pia unaweza kutafuta sabuni ya ukwaju na ukawa unanawa uso asubuhi na jioni hii huondoa upele, chunusi na mabaka usoni

NJIA ZA ASILI ZA KUONDOA MIKUNJO USONI.
kumekuwa na dhana kwamba uwepo wa vipodozi vya kuondoa mikunjo ya ngozi ni wa miaka ya hivi karibuni, la hasha ukweli ni kwamba krimu za kuondoa mikunjo zilitengenezwa kwa mara ya kwanza huko Misri enzi hizo.
kuna njia rahisi sana ambazo zina uwezo wa kutatua tatizo la mikunjo bila kuhaha katika maduka ya vipodozi kutafuta losheni au vipodozi ili kukabiliana na tatizo hili. Sasa unaweza kutumia vitu vya kawaida kabisa kuondoa mikunjo kwa urahisi na kuufanya uso wako uonekane kijana zaidi. Baadhi ya njia hizi ni kama;
Kutumia tango,yai na limao
- vijiko 2 vya juisi ya matango
- ute mweupe wa yai
- kijiko kimoja cha maji ya limao
Maandalizi:
changanya vitu hivyo kwenye chombo kimoja na hakikisha kwamba vitu vyote vimechanganyika sawasawa. Hifadhi mchanganyiko huo tayari kwa kuupaka kwenye uso.TANGO |
LIMAO |
UTE MWEUPE WA YAI |
Jinsi ya kutumia:
- osha uso wako kwa maji na sabuni na hakikisha umeukausha baada ya kuosha uso wako
- pakaa mchanganyiko wako ulioandaa kwenye uso wako na acha mchanganyiko huo bila kunawa kwa muda wa dkk 15 hadi 20 kabla ya kuosha uso wako
- osha uso wako kwa kutumia maji ya uvuguvugu
MWANAMKE MREMBO KUKABILIANA NA TATIZO LA KUOTA NDEVU KWA KUFANYA HAYA.
Mwanamke Kabiliana na Tatizo la Kuota Ndevu kwa Kufanya Haya
Wasichana wanapoota ndevu nyingi
hukabiliwa na changamoto za kisaikolojia na ulimbwende. Mitazamo na mila nyingi
za kijamii katika bara la Afrika, bado zinakumbatia unyanyapaa wa wazi au wa
kificho kwa wasichana wanaoota ndevu nyingi. Msichana mwenye ndevu nyingi
anavuta hisia na macho ya wanaume na wanawake wenzake pia kiasi kwamba
anatazamwa kwa namna ambayo wakati mwingine inamnyima raha. Wakati mwingine
wanaume hawapendi kuoa wasichana wenye ndevu nyingi kutokana na mwonekano
unawafanya wasichana hao kuwa kama wanaume.
Katika hali ya kawaida msichana anatazamiwa asiwe na nywele nyingi kwenye kidevu, juu ya mdomo wake, kifuani, tumboni na mgongoni. Na hata akiwa nazo basi ziwe malaika zisizokuwa na rangi nyeusi iliyokolea na kuwa ngumu kama za wanaume.
Mwanamke anapokuwa na nywele nyingi sehemu hizo humaanisha kuwepo kwa hitilafu za kijenetiki au dosari za ulinganifu wa vichocheo vya jinsia mwilini mwake. Wasichana wengine maumbile yao yanayotokana na vinasaba yanawafanya wawe na nywele nyingi mwilini, hali hii kitabibu hujulikana kama ‘hypertrichosis’.Dosari za ulinganifu wa vichocheo vya kijinsia kwa wasichana zinaweza kusababishwa na:-
(1) Kuzalishwa kwa wingi kwa vichocheo vya ujinsia toka katika mifuko ya mayai.
(2) Uvimbe katika mifuko ya mayai (ovarian tumors)
(3) Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango zenye vichocheo pia zinaweza kuwa chanzo cha tatizo hili kwa baadhi ya wasichana. Dawa hizi husababisha ongezeko la vichocheo bandia vya ujinsia kuwa vingi katika mwili wa msichana.
(4) Matumizi ya dawa na vipodozi vyenye viambato vya dawa kama testosterone na steroid zingine pia husababisha tatizo hili endapo dawa hizi zitatumiwa kwa muda mrefu.
(5) Uvimbe wa tezi ya Adrenali iliyo juu ya figo pia unaweza kusababisha tatizo hili.
(6) Unene wa kupindukia (obesity) kwa wasichana pia unaweza kusababisha ongezeko la kichocheo cha kiume (Androgen) mwilini mwa msichana kutokana na nyama zenye mafuta mengi kugeuza kichocheo cha kike cha estrogen kuwa kichocheo cha kiume cha androgen. Androgen inapokuwa nyingi mwilini husababisha msichana kuwa na tabia za kiume ikiwa ni pamoja na kuota ndevu na kuwa na sauti nzito.
(7) Matumizi makubwa na holela ya baadhi ya dawa zenye kemikali kama vile Danazol, Cyclosporin na zingine pia husababisha tatizo hili.Ni vizuri kwa wasichana kuepuka matumizi ya dawa bila kupata ushauri wa kitabibu.
(8) Ikumbukwe kuwa wakati mwingine kunakuwepo na hali ya ulinganifu wa vichocheo vya ujinsia mwilini kama kawaida, lakini tatizo likawa ni mwitikio wa hali ya juu wa nywele (oversensitivity) kwa kiasi cha kawaida cha kichocheo cha kiume kilichoko mwilini mwa msichana (androgen).Katika hali hii, msichana pia anaweza kuwa na nywele nyingi mwilini kuliko kawaida.
Dalili
zinazo ambatana na kuota ndevu kwa msichana
• Kuota chunusi nyingi.
• Kutokupata damu ya hedhi kama kawaida. Wakati mwingine msichana hupata damu pungufu sana, kutoiona kabisa au kupata hedhi yake bila mpangilio maalumu.
• Matatizo mengine yanayosababisha ndevu kuota kwa wingi pia yanaweza kusababisha ugumba (kushindwa kupata ujauzito na kuzaa watoto).
• Kusinyaa kwa matiti na mfuko wa mji wa mimba.
• Kututumuka na kunenepa kwa kinembe kuliko kawaida (enlargement of the clitoris).
• Kuwa na sauti nzito na wakati mwingine kisanduku cha sauti (Adam’s apple) hunenepa kama cha wanaume.
• Mtawanyiko wa nywele mwilini huwa kama wa kiume, pamoja na ndevu msichana huota nywele kifuani, tumboni, mapajani, mgongoni, miguuni na mikononi kwa wingi. Wengine pia huota nywele nyingi kwenye makalio na kuzunguka sehemu ya njia ya haja kubwa na hali hii ya msichana kuwa na nywele nyingi mwilini, hujulikana kama “hirsutism”.

Jinsi msichana anavyoweza kukabiliana na tatizo la ndevu
• Kwanza kabisa msichana anatakiwa
kuelewa kuwa kuota ndevu sio dhambi na wala si kosa, hivyo basi ndevu zisiwe
chanzo cha msongo wa mawazo.• Msichana asiache ndevu zikawa ndefu kama za wanaume kwani zinavuta hisia za watu kumwangalia angalia kiasi kwamba zinaweza kusababisha matatizo ya kisaikolojia. Ndevu zikatwe na kuwa fupi kadri inavyowezekana kwa wakati wote. Mkasi au cream ya kuondoa nywele inaweza kutumika kwa lengo hili. Ile dhana ya wanawake wengi kwamba ndevu zikinyolewa zinaongezeka maradufu haina ukweli wowote wa kisayansi.
• Ni bora wasichana wakajiepusha na matumizi ya vipodozi vyenye viambato vyenye dawa za magonjwa ya ngozi.
• Ndevu zising’olewe kwa vidole, hii inaweza kusababisha uambukizo wa bakteria katika ngozi kwa urahisi na kuleta matatizo ya kiafya.
• Wasichana waepuke matumizi ya dawa zenye steroid bila kupata ushauri wa kitaalamu toka kwa wahudumu wa afya na maswala ya tiba.
• Kufanya mazoezi ya mwili na kudhibiti unene wa mwili pia husaidia katika udhibiti wa tatizo hili.
• Endapo nywele zimetapakaa kwa wingi miguuni na mikononi na kuleta muonekano wa kiume ni bora kuvaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri ili kuepuka msongo wa kisaikolojia ambao unaweza kutokea kutokana na mtazamo hasi wa kijamii.
• Wakati wote jivunie kuwa msichana, usikubali kitu chochote kikuondolee hisia zako za kuwa msichana kamili. Afya ya mwili na roho huanza na afya ya akili. Jitambue, jipende, jiheshimu na jiamini kwani wewe ni msichana kama walivyo wasichana wengine.
RANGI SAHIHI WAKATI WA KUJIREMBA
YAPO mambo mabalimbali katika tasnia ya urembo hasa katika vipodozi yanayopaswa kuzingatiwa katika kuboresha muonekano wa mtu.
Moja ya mambo hayo ni ujuzi na uelewa wa kutumia rangi katika kujipodoa kwani ni wanawake wachache wenye ujuzi huu.
Katika makala hii, nitakuelezea namna ya kuchanganya na kutofautisha rangi za vipodozi, lengo likiwa ni kuboresha muonekano wako.
Uchanganyaji wa rangi za vipodozi ni muhimu sana kwani katika kujipodoa, rangi zote za vipodozi unavyopaka zinatakiwa zioane ili kuleta muonekano ulio sawa na wa kueleweka.
Kwanza kabisa unatakiwa uwe makini katika kuoanisha rangi za vipodozi pamoja na rangi ya ngozi yako, hivyo katika hili unatakiwa kuwa na ujuzi maalumu ili usije ukafanya makosa na kuharibu muonekano wako.
Pia inabidi ufahamu hatua za upakaji vipodozi ili usije ukafanya vipodozi vingine visionekane katika uso wako.
Namna ya kuoanisha na kutofautisha rangi
Siku zote vipodozi vyako lazima viendane na mavazi yako ili kuleta maana zaidi kwa mfano, mara nyingi rangi ya mdomo ‘lipstick’ huendana na vazi lako wakati shedo ‘eye shadow’ zinatofautiana.
Kwa nguo za pinki
Katika mavazi haya, unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya pinki ambayo itaendana sawasawa na mavazi yako huku ukichanganya na shedo ‘eyeshadow’, inaweza kuwa ya rangi ya bluu ili kuitofautisha na mavazi yako, hapo utakuwa sawa katika kanuni za urembo.
Vazi la kijani
katika vazi hili unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya kahawia huku ukichanganya na shedo ya rangi ya kijani au kahawia iliyoingiliana na pinki au rangi ya machungwa.
Kwa vazi la njano au kahawia
Katika vazi hili unatakiwa kupaka ‘lipstick’ ya rangi ya kahawia iliyokolea, kwa upande wa shedo waweza kupaka ya rangi ya dhahabu.
Kwa vazi la bluu
Katika vazi hili unatakiwa kupaka ‘lipstick’ yenye rangi ya pinki huku ukipaka shedo ya rangi ya bluu kwa mtindo huu utakuwa mwenye kuvutia siku zote.
Subscribe to:
Posts (Atom)